Utangulizi wa Imani ya Kibaha’i
Katika historia, Mungu amekuwa akituma kwa binadamu
mlolongo wa Waelimishaji watakatifu —wajulikanao kama
Wadhihirishaji wa Mungu — ambao mafundisho yao
yametoa msingi kwa ajili ya uendelezaji wa ustaarabu.
Wadhihirishaji hao hujumuisha Abraham, Krishna,
Zoroaster, Moses, Buddha, Jesus, na Muhammad.
Bahá’u’lláh, mtume wa sasa miongoni mwa hawa,
alieleza kuwa dini za ulimwengu zimekuja kutoka Chanzo
kimoja na kwa asili katika mfuatano wa kurasa za dini
moja kutoka kwa Mungu.
Uwepo wa Wa-Baha’i Tanzania
WaBahá’í huamini kuwa hitaji muhimu linaloikabili binadamu ni utafutaji wa muono wa pamoja wa jamii ya wakati ujao na asili na makusudi ya maisha. Muono kama huo unakunjuka katika maandiko ya Bahá’u’lláh.
Wa-Baha’i wa Tanzania
Mnamo 1950 Imani ya Baha’i ilikuja Tanzania. Leo wapo Wa-Baha’i katika takriban maeneo 3000 kila mahali nchini, na zaidi ya halmashauri 150 za Kiroho za Mahali ambazo zinaitwa Mabaraza ya Kiroho ya Mahali. Wa-Baha’i huamini katika elimu ya wote na utokomezaji wa ubaguzi wa aina zote, kama ni wa mbari, kabala, kitaifa, kidini au ya usuli wa kijamii.
Wa-Baha’i huendesha madarasa ya watoto juu ya elimu ya sifa njema na maadili ya mtu; mikutano ya ibada,; na vikundi vya mafunzo kwa ajili ya watu wazima na vijana juu ya mada za kiroho. Wa-Baha’i wa Tanzania wanaendesha Shule ya Sekondari ya Ruaha huko Iringa pamoja na shule nyingine nyingi katika jumuiya za kila mahali nchini.